KUNDI la wanachama wa klabu ya Yanga (Pichani) wameishika pabaya kamati ya ligi pamoja na shirikisho zima la kandanda nchini TFF kwa kitendo chao cha kuilazimisha klabu yao kuukabali udhamini wa Azam Media.
Wakizungumza jana kwa nyakati tofauti wanachama hao wamedai kuwa kamati ya ligi kwa kushirikiana na TFF ni wababaishaji katika mpango mzima wa kutaka kusaini mkataba wa miaka mitatu na Azam TV ambayo mpaka sasa haijulikani hata ofisi zake zilipo.
Pia wanachama hao wanashangaa kuona viongozi wa kamati ya ligi ambao wamebakiza miezi miwili kuondoka madarakani wanasaini mkataba mrefu na kampuni isiyoanza hata majaribio.
Wamedai televisheni zote zinazoanza kuonekana mbele ya jamii zinapewa miezi mitatu kwa ajili ya majaribio iweje TFF iwaidhinishe Azam kuonyesha ligi wakati hata kipindi cha kuonyesha katuni hawajaanza.
Yanga imekuwa katika malumbano makali na kamati ya ligi baada ya kupinga kuonyeshwa kwa mechi zao kwa madai kuwa Azam na Yanga ni mahasimu