come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

BIN KLEB AIPIGA BAO JINGINE SIMBA.

Kukiwa na tetesi kwamba viongozi wa Simba wapo katika mpango wa kuwanyemelea beki Kelvin Yondani na kiungo Simon Msuva kwa ajili ya kuwasajili msimu ujao, uongozi wa Yanga umeanza mchakato wa kuwapa mikataba mipya wachezaji hao.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, mwenyekiti wa Kamati ya usajili ya klabu ya Yanga, Abdallah Bin Kleb alisema wameanza mchakato wa kuwasainisha mikataba mipya wachezaji hao.

Bin Kleb alisema kuwa timu hiyo bado inahitaji huduma za wachezaji hao hivyo watawasainisha mikataba mipya muda mfupi kuanzia sasa ili waendelee kuitumikia Yanga.

Mikataba ya Yondani, aliyesajili na Yanga akitokea Simba 2011, na Msuva aliyetoka Moro United inamalizika mwisho mwa msimu huu wa ligi kuu ya Bara.

Kwa kutambua mikataba hiyo inafikia tamati ndani ya miezi sita ujayo hivyo kuwafanya wawe katika nafasi ya kuingia makubaliano mapya na timu yoyote, viongizi wa Simba walianza mipango ya siri ya kuwasajili wachezaji hao, imedaiwa.


“Tunajua sio Simba tu... kutakuwa na timu nyingine ambazo zinaweza zikawa zinawawinda wachezaji hawa (hivyo) tayari tumeanza mchakato wa kuwasainisha mikataba mipya na muda wowote watasaini,” alisema Bin Kleb.