come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

LIGI KUU MPYA KUANZA MWAKANI.

Tanzania students Beach Soccer League imekusidia kuanzisha mchezo wa mpira wa miguu ambao unachezwa kwenye fukwe za bahari ambayo itakusanya timu za vyuo vikuu zote na kushindana ili kupata mshindi na pia kutengeneza timu ya taifa ya vyuo vikuu.

Uzinduzi wa ligi hii utafanyika mwishoni mwa mwaka huu na timu za vyuo zitashindana katika bonanza la siku mbili kwenye fukwe za bahari ya hindi na mwanzoni mwa mwaka 2014 ndipo ligi kuu ya mpira huu
itafanyika na kushirikisha vyuo vikuu vyote nchini.Mchezo huu unasimamiwa na kampuni ya Plan B Solutions (T) ltd ambayo ina makazi yake Dar es salaam, Tanzania.

Kuanzishwa kwa mashindano haya ya ligi ya wanafunzi ya ufukweni inalengo la kuendeleza mawasiliano ya karibu, ushirikiano na nidhamu zakuimarisha kwa vijana wa taifa letu.

'Tutatoa msaada wa kuifundi kwa washiriki kupitia makocha na wakufunzi wetu waliopata mafunzo kutoka kwa wakufunzi wa FIFA Beach Soccer na hii yote ni kuwa na lengo la kupata wachezaji watakaounda timu ya taifa na vilevile kupata wachezaji watakao shiriki ligi kuu ya soka la ufukweni', ilisema taarifa ya waandaaji.


'Plan B Solutions (T) ltd imedhamiria kukuza na kuendeleza soka letu la ufukweni ndani na nje ya Tanzania na kutoa msaada wa hali na mali ilikuweza kufanikisha ndoto za vijana wengi wenye vipaji. Kupitia mipango
maalumu tutaendelea kutoa mafunzo na elimu kuhusu hii soka la ufukweni kuanzia marefa, makocha,wachezaji wa kiume na wanawake,kutoa semina za mchezo, vifaa vya kuchezea, na msaada wa kisheria na taratibu za FIFA.