come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

CASILLAS WA MTIBWA AITOSA SIMBA.

Kipa wa kutumainiwa wa Mtibwa Sugar, Hussein Sharrif 'Casillas' amesema yupo tayari kutua Msimbazi ili kuitumikia klabu ya Simba ambayo imeonyesha nia ya kumsajili.

Akizungumza jana, Casillas alisema yapo mazungumzo yaliyowahi kufanywa baina yake na uongozi wa Simba, lakini hafahamu kama klabu hiyo inamtaka kweli au ilikuwa 'inam-beep'.

Kipa huyo wa zamani wa Villa Squad, alisema hakuna mchezaji asiyependa kuchezea timu kubwa kama Simba na kwamba yupo tayari kutua Msimbazi.

Casillas alisema anaamini uwezo mkubwa alionao unamruhusu kuidakia Simba iwapo itakuwa na dhamira ya kweli ya kumchukua kwa ajili ya duru la pili la ligi kuu ya Bara.

"Kumekuwa na mazungumzo na uongozi wa Simba juu yangu kwa siku za nyuma, lakini mpaka sasa sijasikia chochote," alisema. "Kama kweli wananihitaji mimi nipo tayari kutua Msimbazi na kuidakia.


"Hakuna asiyependa kuidakia timu kubwa kama Simba, (na) wakimalizana na klabu yangu nitatua kwao na kuidakia kwa mafanikio. Najiamini ninaweza."

Simba imekuwa ikihusishwa kumnyemelea kipa huyo kutokana na madai ya uongozi kutorodhishwa na uwezo wa Abel Dhaira kutoka Uganda.

Mbali na Casillas, Simba imekuwa ikidaiwa pia kutaka kumsajili kipa wa zamani wa Yanga na Prisons aliyerejea Taifa Stars baada ya kufanya vyema katika ligi kuu ya Kenya akiwa na Gor Mahia, Ivo Mapunda.