Kigezo Zlatan Ibrahimovic nusura apasuwe wavu na
kombora kali lililokita mzizi kimyani pale wageni PSG wa Ufaransa
walipowabwaga wabambe wa Ujerumani, Bayer Leverkusen, 4-0 katika mkondo
wa kwanza wa awamu ya mwondoano katika shindano la UEFA Champions League
Jumanne.
Mshambuliaji huyo wa Uswidi pia alifunga penalti na kuandikisha bao lake la kumi musimu huu katika shindano hilo dakika mbili kabla ya mechi kutamatika baada ya Blaise Matuidi, kufungulia Wafaransa hao udhia mapema dimba hilo.
Yohan Cabaye aliongezea la nne dakika mbili kabla ya kipenga cha mwisho huku Leverkusen, waliofedheheshwa 5-0 nyumbani na mabingwa wa Uingereza, Machester United katika shindano hilo, wakikosa jibu la mashambulizi ya wageni wao.
Mashaka ya Leverkusen yalisomba pale Emir Spahic alipoamrishwa kuaga mechi hiyo dakika ya 59 kwa kosa la kupokea kadi yake ya pili ya njano.
Leverkusen, wanaobobea katika nafasi ya pili katika ligi kuu ya Ujerumani, Budesliga, walijipata taabani sekunde chache baada ya kipenga cha ufunguzi pale nahodha wao, Simon Rolfes, alipopoteza mpira kwa Matuidi.
Mfaransa huyo alimwadhibu vikali pale alipojongelea eneo hatari na kumimina mkwaju mkali uliofungua orodha ya mabao baada ya kubadilishana pasi za haraka na wenzake Marco Verratti na Ibrahimovic kabla ya kulemea kipa mpinzani.
Wageni walijipata 2-0 dakika ya 39 pale Saphic alipopatiana penalti kwa kuchezea straika Ezequiel Lavezzi makosa eneo la hatari na Ibrahimovic akaziba adhabu hiyo kimyani.
Dakika tatu baadaye, Ibrahimovic alifunga bao spesheli kama ilivyo uzoefu wake pale alipoelekeza mpira pembeni mwa neti pale alipopokea pasi kutoka Matuidi licha ya kuwa alikuwa anakosa mwelekeo baada ya kujipinda.
Cabaye alifunga udhia na kombora rojo rojo liliomwacha kipa Leno bila jibu.