Na Mc DogoTano
MABINGWA wa soka nchini Yanga wamewaambia mashabiki wao kwamba hawatawaangusha hata kidogo katika kampeni yao ya kutetea ubingwa wa bara na sasa wamewapigia mahesabu makali wanajeshi wa Ruvu Shooting kutoka Ruvu Mlandizi Pwani.
Akizungumza na Staa wa Leo kwa njia ya simu msemaji wa Yanga Baraka Kizuguto amesema kuwa kikisi cha Yanga hakitafanya makosa hata kidogo kupoteza mchezo wowote wa ligi kuu bara,Yanga inajiandaa vikali kuibuka na ushindi tena mnono dhidi ya Ruvu Shooting.
Timu hizo zinakutana mwishoni mwa wiki hii ambapo Ruvu Shooting imeanza tambo kwamba itaibuka na ushindi ili kudhihirisha kuwa wao ndio kiboko ya timu zilizofanya ziara nje ya nchi msimu huu,tayari Ruvu ilifanikiwa kuibuka na ushindi dhidi ya Coastal Union ambao waliweka kambi yao Oman.
Yanga iliweka kambi yake Uturuki, inatarajia kukutana na upoinzani mkali kutoka kwa wanajeshi hao,jana msemaji wa Ruvu Shooting Masau Bwire alisikika akitamba redioni kuwa timu yake itaifunga Yanga, mbali ya kujitamba pia alitoa maneno ya kashfa kwa Yanga kuwa timu waliyocheza nayo katika michuano ya kimataifa ya Komorozine ya Comoro ni sawa na timu ya kijijini kwake ya Mkulima FC