come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

176 WADAIWA KUFA BAADA YA MAPOROMOKO MAREKANI

Athari ya maporomoko Marekani
Maafisa wa utawala katika jimbo la Washington nchini Marekani, wamepata miili sita zaidi baada ya maporomoko ya ardhi yaliyotokea siku ya Jumamosi.

Hii imefikisha idadi ya watu waliofariki kutokana na maporomoko hayo hadi 14.
Watu 176 bado hawajapatikana baada ya ukuta wa matope wenye urefu wa futi 177 kuporomoka karibu na mji wa Oso, Kaskazini mwa Seattle.


Waokozi wangali wanaendelea na shughuli ya kuwatafuta manusura kwa kutumia helikopta na miale ya Laser.

Lakini maafisa wanakiri kuwa wana matumaini madogo sana ya kupata manusura.
Rais Barack Obama ametangaza hali ya hatari katika jimbo hilo na kuwaamuru maafisa wote wa serikali ya jimbo hilo kushirikiana kutoa msaada wa dharura.

Gavana wa jimbo hilo ameitaja hali kuwa mbaya na ambayo haikutarajiwa.
Watu 176 bado hawajapatikana.

Jamaa na marafiki pamoja na wafanyakazi wa kujitolea, wanatumia misumeno na mikono mitupu kuondoa vifusi ili kutafuta wale waliopotea.