come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

HASIRA ZETU TUNAZIELEKEZA KWA MTIBWA- PLUIJM

Yanga SC ambao ni mabingwa wa Bara wamekubali matokeo na wamerejea Tanzania kuelekeza nguvu zao katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, ili watetee ubingwa wao, ambako wanatarajiwa kuelekea mjini Morogoro.

Kocha Mkuu wa klabu hiyo, Mholanzi Hans Van der Pluijm alisema kwamba vigogo wa Misri Al Ahly wamepoteza makali yao na si timu tishio tena ile aliyokuwa anaijua yeye, licha ya kuitoa timu yake juzi kwa penalti mjini Alexandria.

“Ilivyo, Al Ahly hii si timu kali tena ambayo sote tulikuwa tunaijua na ikiwa wataendelea kucheza kama hivi katika hatua ijayo, nina uhakika watataabika,”.

“Tulikuwa karibu kuwatoa nje ya mashindano, lakini penalti ni mchezo wa bahati, na ninajivunia kiwango chetu,”alisema Pluijm baada ya mechi juzi.


Baada ya kuitoa Yanga SC, timu hiyo yenye maskani yake mjini Cairo itakutana na Al Ahly Benghazi kuwania kuingia Hatua ya makundi ya michuano hiyo.

Yanga SC ambayo katika Ligi Kuu ya Bara inakabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa Azam FC katika mbio za ubingwa, itamenyana na Mtibwa Sugar Uwanja wa Jamhuri, Morogoro Jumamosi.

Yanga SC inashika nafasi ya tatu katika Ligi Kuu kwa pointi zake 38 kutokana na mechi 17, nyuma ya Mbeya City yenye pointi 39, baada ya kucheza mechi 21, wakati Azam ipo kileleni kwa ponti zake 40 baada ya mechi 18.

Akielezea mchezo huo na Mtibwa, Pluijm amesema anakwenda kuzoa pointi tatu kwakua kikosi chake kiko kamili na kinaonyesha ushindani halisi, amedai Mtibwa si timu bora kama Yanga lakini anaiheshimu.