Na Salum Fikiri Jr
ELIAS Jonh January hatimaye hivi karibuni aliachana na klabu ya ukapera na kuamua kufunga pingu za maisha na Bi Martha Myurra katika kanisa la Mtakatifu Joseph lililopoPosta jijini Dar es Salaam na kufuatiwa na hafra kubwa iliyofanyika Mbezi Garden katika ukumbi mdogo wa Serengeti Hall.
Kwa mujibu wa shuhuda wetu aliyekuwepo katika tukio hilo Elias na Bi harusi (Pichani) waliweza kutimiza azma yao hiyo baada ya kuisubiria kwa kipindi kirefu, akizungumza kwa furaha, bwana harusi ambaye pia ni mwandishi wa kujitegemea amesema amefurahi vya kutosha kuuaga ukapera.
Amedai ukapera ulikuwa ukimsumbua sana hivyo kuachana nao amefurahi, anawasifu ndugu, jamaa na marafiki waliojitolea kwa hali na mali kumsaidia kufikia azma yake hiyo, naye bi harusi amesifu tukio hilo na kuliiita la kihistoria.
Bwana harusi kwa sasa ni mfanyabiashara, wakati bi harusi ni mfanyakazi serikalini,wote kwa pamoja wameanza maisha mapya ndani ya ndoa, mungu wabariki