MABINGWA wa soka nchini Yanga, wametamba kuchukua ubingwa msimu huu tofauti na mawazo na mategemeo ya wapenzi wa soka nchini ambao wanaipa nagfasi kubwa Azam FC kutwaa ubingwa huo, katibu mkuu wa Yanga Benno Njovu amesema ubingwa uko palepale kwa Yanga.
Akizungumza na mtandao huu, Njovu ameonekana kuwashangaza wengi kwa kudai Simba na Mmbeya City ndizo zitakazoitangazia Yanga ubingwa, ameongeza kuwa ni mapema kuitangaza Azam mabingwa wakati haijamaliza shughuri.
Shughuri ni pevu Azam bado haijakutana na timu ngumu kama za Mbeya City, Mgambo JKT na Simba ambapo kama itazifunga timu hizo basi nawatangaze ubingwa, alisema Njovu, aidha amedai kikosi chake kimedhamilia kutwaa ubingwa msimu huu na ndio maana kilikwenda kuweka kambi nchinini Uturuki.
Ametamba Yanga ina kikosi kizuri pengine kuliko timu zote zinazoshiriki ligi hiyo isipokuwa imepitwa na Azam kwa tofauti ya pointi nne,'Wengi hawajui kama tulisimama kucheza mechi za ligi kwakuwa tulikuwa tunaliwakilisha taifa,hivyo tumerejea ligi kuu na kila anayekatiza mbele yetu ni kipigo tu', aliongeza Njovu.
Yanga ilifikisha pointi 42 ikiwa na mechi 20 baada ya kuifanyia kitu mbaya Rhino Rangers ya Tabora katika uwanja wa Ally Hassan Mwinyi, katika mchezo huo kikosi cha Yanga kilishinda mabao 3-0 yaliyowekwa kimiani na Jerry Tegete aliyefunga mawili na Hussein Javu