Steven Gerard alifunga mikwaju
miwili ya penalty na kukosa ya tatu Liverpool ikiendelea kuimarisha
matokeo yake baada ya kuwacharaza mabingwa watetezi wa ligi ya uingereza
Machester United tatu bila katika uga wao wa nyumbani Old Trafford.
Nahodha wa Liverpool Gerard alionyesha uongozi wake huku wakifazawadiwa mikwaju ya penalty katika vipindi vyote viwili huku timu hiyo ya meneja Brenda Rodgers ikitawala dhidi ya timu ya Machester ambayo inahitaji marekebisho makubwa.
Kutokana na mechi hizo za leo Chelsea iko katika nafasi nzuri ya kushinda taji hilo kwa alama 66 ikiwa imecheza mechi 30 huku timu za liverpool na Arsenal zikiwa na pointi 62 kila mmoja, lakini liverpool inashikilia nafasi ya pili kwa wingi wa mabao.
Arsenal ni ya tatu huku Manchester City iliocheza mechi 27 ikiwa na pointi 60 na hivyobasi ikifunga udhia wa time nne bora.