Wawakilishi wa Morocco, Difaa Hassani El Jadida walikuwa kwenye nafasi ya kusonga mbele baada ya mabao ya kipindi cha pili ya Ahmed Chagou na mchezaji kutoka Gabon, Johan Lengoualama, kabla ya Raouf kufunga dakika ya mwisho na kuivusha Ahly.
Kwa matokeo hayo, Ahly inasonga mbele kwa faida ya bao la ugenini kufuatia awali kushinda 1-0 nyumbani hivyo kufanya sare ya jumla ya 2-2.
Katika mechi nyingine za juzi, Bayelsa Utd ya Nigeria ilifungwa 1-0 nyumbani na Sewe Sport ya Ivory Coast na kutolewa kwa jumla ya mabao 2-0.
Mechi nyingine zilichezwa jana, AS Real na Djoliba zote za Mali, AC Leopards ya Kongo na Medeama ya Ghana, Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini na ASEC Mimosas ya Ivory Coast, Coton Sport ya Cameroon na Petro Atletico ya Angola, Horoya ya Guinea na Etoile du Sahel ya Tunisia na Nkana FC ya Zambia na Club Athletique Bizertin ya Tunisia
CHANZO BIN ZUBEIRY BLOG