come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

KAOLE YAREJEA KWA KASI MPYA

Na Regina Mkonde

Kundi la zamani la sanaa linalofahamika kwa jina la Kaole Sanaa Group hivi karibuni lilijiunga na kudai kuwa lipo njiani kurudisha hadhi ya sanaa nchini.

Maneno hayo yalielezwa na baadhi ya wasanii waliopo katika kundi hilo walisema kwamba lengo la kurudi kwa kaole katika tasnia ya tamthiliya lilikuja mara baada ya kuona hadhi ya sanaa inazidi kushuka siku hadi siku bila sababu ya msingi.

Mnamo mwaka 1996 kundi hilo lilianza kuvuma kupitia tamthiliya yao ya hujafa hujaumbika iliyokuwa ikirushwa katika chaneli ya ITV lilikufa kutokana na sababu iliyokuwa nje ya uwezo wao iliyosababishwa na uongozi kutozingatia taratibu za kundi hilo.


Mmoja kati ya wasanii wa kundi hilo ambaye hakutaka jina lake litajwe alidai kuwa toka uongozi mpya ulivyoingia wasanii tulikuwa hatuthaminiwi na wakati mwingine haki zetu tulikuwa hatupewi ndiyo maana baadhi ya wasanii tuliamua kujitenga na hatimaye kundi hilo kuvunjika.

Yapata miaka 10 toka kundi hilo lififie na kuwa kimya katika tasnia ya tamthiliya kabla ya kundi hilo kufa kulikuwa na tamthiliya ambayo walitaka kuirusha katika chaneli ya TVT ambayo kwa sasa inaitwa TBC jitihada zao zilikwamishwa na utawala mbovu wa uongozi mpya.

Kundi hilo ambalo apo awali lilikuwa makao makuu yake maeneo ya lango la jiji katika ukumbi wa Anex jijini Dar es salaam hivi sasa baada ya kuungana upya wameweka kambi katika ukumbi wa Dar Modern Taarab uliopo maeneo ya magomeni mikumi Dar es salaam.

Kaole Sanaa Group sasa limebadilika na kuitwa Kaole Kwanza nia na madhumuni ya kujiunga tena ni kuhakikisha kwamba hadhi ya sanaa hususani Tamthiliya inarudi tena hali hii imetokea baada ya  wasanii wachanga kudumaza hadhi ya sanaa kwa kutozingatia maadili na taratibu za sanaa,kwa sasa hakuna Tamthiliya toka kipindi cha nyuma tulipoacha kuigiza hakuna tamthiliya zenye viwango hapa nchini yaani sisi tuliondoka na sanaa alisema mwanachama wa kundi la Kaole kwanza.

Kwa sasa sanaa haina hadhi hii yote imesababishwa na watu wachache wasio na uelewa wa sanaa baadhi ya watu hawaangalii uwezo ama kipaji cha mtu bali huangalia umaarufu uzuri na hata shepu wakiamini kuwa ndiyo sanaa itaendelea na kupata mashabiki wengi hii si sahihi maana inaua vipaji sababu wapo wenye vipaji hawachukuliwi kisa hawana mvuto na umaarufu pia  taswira hii ndiyo iliyoharibu hadhi na soko la sanaa hapa nchini.

Apo awali mtu huwezi kuigiza ikiwa huna kipaji cha kuigiza mtu unaweza kusota hata miezi kadhaa bila ya kuoneka kama utakuwa hujafuzu mazoezi ila kwa sasa mtu ukipata umaarufu wa jambo fulani unaweza ukaigiza,hii siyo nzuri na inawaumiza wale ambao wenye vipaji mwanamuziki abaki na uwana muziki wake endapo ataona kuigiza hawezi na hata kwa wengine pia wasilazimishe fani ambazo si za kwao maana wanatuharibia kazi zetu.Walisema wasanii wa kundi hilo.

Pia waliongeza kuwa hivi sasa utamaduni wetu hatuuzingatii ndiyo maana tamthiliya nyingi na filamu utakuta wanonyesha mandhari ya mjini tu hata wakati mwengine wanaiga destuli za wenzetu inabidi tuitangaze nchi yetu kwa kuigiza hali halisi ya utamaduni wetu na tuachane na kuiga mila za wenzetu maana hii inatuumiza.

Ukiangali wenzetu wana igeria wanaitangaza nchi yao kwa kuigiza maisha yao halisi na kuonyesha mila na destuli zao hali hii kwetu imekuwa kinyume tunavaa mavazi ya kigeni na hata kuiba ujuzi wa wenzetu.


Ina bidi watanzania tubadilike na tuachane na tabia ya kuiga na kuiba kazi za wenzetu utakuta filamu ya hapa nchini inafanana na filamu ya nje kimaudhui na kila kitu inabidi tubadilike na kuwa wabunifu wa kutunga kazi zetu wenyewe na tuache kuiba aidia za wenzetu kama baadhi ya wasanii wafanyavyo.

Kaole kwanza hivi sasa ipo kwenye mataarisho ya kutoa tamthiliya yao mpya inayotarajia kutoka hivi karibuni inaitwa Kipusa licha ya hivyo mpaka sasa hawajafahamu tamthiliya hiyo itarushwa stesheni gani.