come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

DIDA ASEMA YEYE NA YANGA NI DAMU DAMU

MLINDA lango wa kutegemewa na Yanga Deogratus Munishi 'Dida' amekanusha vikali taarifa iliyolewa na vyombo vya habari kuwa ana mipango ya kutimka katika kikosi hicho cha Wanajangwani, Dida amesema yeye ni mchezaji wa Yanga na ataendelea kubakia Yanga.

'Nimepata mafanikio makubwa nikiwa na Yanga hivyo sioni umuhimu wa kuondoka kikosini hapo, nina imani na Yanga na wala sifikirii kuondoka', alisema Dida, baadhi ya mitandao ya kijamii jana na leo (Siyo Mtandao huu) na magazeti yameandika taarifa za kipa huyo kuwa anataka kuondoka.

Kipa huyo ambaye yuko kwenye kambi ya timu ya taifa iliyopo jijini Mbeya ikijiandaa na mchezo wa kirafiki dhidi ya Malawi 'The Flame' utakaopigwa uwanja wa Taifa jumamosi inayo amedai Yanga ni timu kubwa na yenye mafaniko hivyo hawezi kuondoka kamwe.


'Najiona mtu mwenye bahati tangia nitue Yanga, nilichukuliwa baada ya kutemwa na Azam fc siku na msisimko mkubwa nilipotua Yanga kusema kweli Yanga ilikuwa na kipa chaguo la kwanza Barthez (Ally Mustapha) baadaye akasajiliwa Kaseja (Juma) hivyo maisha kwangu yalikuwa magumu', alisema na kuongeza.

'Mchezo wa mpira ni mchezo wa makosa, ili uanze kikosi cha kwanza lazima mwenzio ateleze, hao ndipo nilipoanza kucheza katika kikosicha kwanza, nashukuru michuano ya kimataifa imenitangaza na sasa ndio kipa wa kwanza wa klabu hiyo pamoja  na timu ya taifa, Taifa Stars.

Aidha kipa huyo amewaomba mashabiki wa Yanga kutoichukulia uzito kauli hiyo kwakuwa ilikuwa na malengo ya kuwagombanisha, anawataka Wanayanga kuwa na imani naye na ataendelea kuitumikia katika msimu ujao wa ligi kuu bara na michuano ya kimataifa.

Pia anasema endapo mipango yake ya kucheza soka la kimataifa Uarabuni itatimia basi anataka auzwe na klabu yake ya Yanga na si timu nyingine