come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

KHEDIRA, SCHWEINSTEIGER WAANZA MAZOEZI UJERUMANI

Sami Khedira

Matumaini ya Ujerumani kuchezesha kikosi kamili katika hali nzuri yalipokea kiinua mgongo Jumatano baada ya viungo Bastian Schweinsteiger na Sami Khedira kuchapa zoezi kwa mara ya kwanza na timu hiyo inayojiandaa Kombe la Dunia.

Kigezo cha Bayern Munich, Schweinsteiger, ametatizwa na majeraha musimu uliopita huku goti lililowasha likiwa la mwisho kumwandama na kumfanya akose mchezo kwa majuma kadhaa yaliopita.

Khedira ambaye alishirikiana na Schweinsteiger kuunda kiungo dhabiti katika michuano ya dunia ya 2006 na 2010 amerejea hivi majuzi baada ya kukosa miezi sita kutokana na kukata kano la goti lake mwaka uliopita.


Amecheza mechi chache tangu kupona, miongoni mwao fainali ya Ligi ya Mabingwa ambayo timu yake Real Madrid ilitamba na alijiunga na wenzake wa Ujerumani Jumatatu jioni.

Wawili hao walionekana kusonga bila shida yeyote uwanjani kwenye kambi yao ya Italia ambapo wananoa makali yao.

Kocha Joachim Loew amebaki na kijasho cha nahodha wake, Philipp Lahm ambaye alifanya mazoezi finyu huku beki aliyejeruhiwa, Marcel Schmelzer, akipsha misuli pekee yake.
Golikipa Manuer Neuer hatoshiriki kwa siku chache zijazo na hatafanya mazoezi Italia anapoendelea kuuguza jeraha la bega.

Ujerumani watagaragazana na Ghana, Marekani na Ureno kwenye Kundi G na watajipima nguvu na Cameroon Juni mosi na Armenia siku tano baadaye kabla ya kusafiri Brazil.