|
|
Mabingwa wa ligi ya Premier, Manchester City,
huenda wakapoteza mchezaji bora zaidi msimu uliopita, kiungo cha kati
Yaya Toure, baada ya staa huyo kueleza ingekuwa ni ‘heshima’ kuchezea
Paris Saint-Germain wa Ufaransa.
Toure, ambaye alichukua usukani wa kuendesha City kunyakua tena taji la Premier alilalamika wiki jana kuhusu vile klabu hicho kilipuuzilia sherehe za siku yake ya kuzaliwa alipogonga miaka 31 na kumkosea hadhi.
Akihojiwa na jarida la France Football lililochapishwa Jumanne, Toure alinukuliwa akisema “Unawezaje kukosa hamu ya klabu chenye malengo kama Paris,” akiongeza, “Itakuwa heshima kuwa sehemu ya timu kama hiyo siku moja.”
Toure alisaini kandarasi ya miaka minne na City mwaka jana.