come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

KIONGOZI WA KANISA ADAIWA KULA SADAKA

Na Regina Mkonde- Nigeria

Mwanzilishi wa kanisa la Faith Chapel la nchini Nigeria hivi karibuni alikuwa na shutuma za kutumia pesa za kanisa vibaya kwa matumizi yake binafsi.

Licha ya shutuma hizo zilizomkuta Askofu mkuu wa kanisa hilo amedai kuwa anafuraha kwa baadhi ya wananchi wanaomshutumu kula pesa za Kanisa mchungaji huyo anadaiwa kununua ndege kwa kutumia pesa za kanisa ambazo waumini walizichanga.

Shutuma za viongozi wa kanisa kutumia vibaya pesa za kanisa hususani za michango na kufanya mambo yao binafsi hali hii si kwa Tanzania tu inatokea hata kwa nchi za wenzetu jambo hili linafanyika viongozi wengi wamekuwa si waaminifu kwa kufuja vibaya mali za kanisa ambazo waumini wanazichanga.


Mchungaji huyo aliyetuhumiwa kwa kutumia mali za kanisa vibaya alijitetea na kudai kuwa kwa wale wot wanaomuamini Yesu Kristo ni haki yao kuwa matajiri sababu alishawabariki tayari na wale ambao hawaamini hujionea wenyewe baada ya kumpokea Kristo hivyo basi mimi sitishikiwanavyoujadili uatajiri wangu bali watazidi kunifurahisha.Alisea mchungaji huyo.

‘Pia sioni haya watu wakiushangaa utajiri wangu maana Mungu ndiye aliye nipa hakuna mtu anayefurahi kuwa masikini kila mtu anachukia kuitwa masikini hakuna anyeufurahia umasikini hata siku moja hata sisi hapo awali tulikuwa masikini lakini kwa aajili ya neno la Mungu tumekuwa matajiri’.

Alizidi kujitetea mchungaji huyoCha ajabu mchungaji huyo alipoulizwa anajisikiaje kwa waumini wake kumtuhumu kwa kosa la kutumia pesa za kanisa na kununua ndege yake binafsi alisema kwamba anajisikia vizuri sana kwa tuhuma zao wanazoendelea kumtuhumu kila mtu anahaki ya kutoa maoni yake juu ya swala hili hivyo basi sishangai na wala sitawakasirikia kwa tuhuma wanazozidi kunipa.

Inavyosemekana mchungaji huyo ilkuwa ni desturi yake kutumia vibaya pesa za kanisa na anapoulizwa hujitetea na kudai kuwa Mungu ndiye aliyempa utajiri huo huku pesa za kanisa zikipotea kimiujiza.

Siku hizi makanisa yamekuwa kama biashara tofauti na hapo awali tena viongozi wao baadhi wamekuwa wajasiria mali kwa kutumia vibaya pesa za Kanisa hususani michango na sadaka kutoka kwa waumini.

Kesi kama hizi zinatokea mara nyingi hata hapa kwetu ila kwenye nchi ya Nigeria tatizo hili limekithiri na ndiyo nchi inayoongoza kwa kuwa na makanisa mengi kwa hapa Afrika.

Kwa mtu mwenye akili timamu hawezi akafurahia tuhuma chafu kama hizo tena ni mwanzilishi wa kanisa hilo na ni mchungaji mkuu.