KIUNGO wa Manchester United, Adnan Januzaj ameichezea mechi ya kwanza Ubelgiji Jumatatu usiku ikiibuka na ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya Luxembourg katika mchezo wa kirafiki ambao mshambuliaji wa Chelsea, Romelu Lukaku alifunga mabao matatu.
Lukaku alifunga bao la kwanza dakika ya tatu, akimalizia pasi ya Marouane Fellaini. Joachim aliisawazishia Luxembourg dakika ya 13, lakini Lukaku akaifungia Ubelgiji bao la pili dakika 10 baadaye.
Nyota wa United, Januzaj alichezea mechi yake ya kwanza kikosi cha Ubelgiji akitokea benchi kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Marc Wilmots, huku Vincent Kompany na Eden Hazard wakipumzishwa.
And Lukaku, ambaye alikuwa kwa mkopo Everton msimu uliopita, alikamilisha mabao yake matatu kabla ya Nacer Chadli kufunga la nne na Kevin De Bruyne kufunga la tano.