come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

MGANGA WA DIAMOND AFICHUA MAKUBWA

Mtu anayedaiwa kuwa ndiye mganga wa mwanamuziki nyota nchini na mshindi wa tuzo saba za Kilimanjaro music Award Nasseb Abdul maarufu Diamond Platinum, Rajabu Kondo ( Aliye pichani) amesema kuwa yeye ndiye aliyemwezesha msanii huyo kufanya vizuri kwa sasa.

Akizungumza na Staa wa Leo nyumbani kwake Bunju B nje kidogo ya Dar es Salaam, Kondo amedai amefanya kazi kubwa kumng'arisha Diamond na aneweza kumbeba na kufanikiwa kuchukua tuzo saba za Kili pamoja na kuingia kwenye tuzo mpya za BET nchini Marekani ambapo sasa msanii huyo wa Tanzania anakutana uso kwa uso na mastaa wa dunia.

Kondo amedai ameweza kukesha na Diamond makaburini ili kumfanyia mambo ambapo alishiriki naye kushiriki ibada mbalimbali za kichawi ilimradi wafanikiwe, 'Namsifu Diamond ni msikivu na mvumilivu, niliweza kukesha naye makaburini kutafuta dawa za mafanikio',alisema na kuongeza.


'Unajua hakuna kinachoshindikana chini ya jua, mimi ni mganga wa kweli na wala sina masihara katika hilo hivyo niliweza kufanya naye kazi vizuri ambapo kufanikiwa kwake ndio kwangu', aliongeza mganga huyo anayesifika kwa kutibu maradhi mbalimbali ikiwemo uchizi.

Aidha mganga huyo alitoa namba zake za simu ili kama kuna wengine wanamuhitaji waweze kumtafuta 0688 904777 ama unaweza kufika ofisini kwake Bunju B nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam