come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

PATRICE EVRA AONGEZA MKATABA MAN UNITED

Patrice Evra 

Beki wa kushoto wa Ufaransa Patrice Evra ametia saini mkataba wa kukaa Manchester United kwa mwaka mmoja zaidi, na kuongeza kipindi chake Old Trafford hadi msimu wa 10, klabu hiyo ya Ligi ya Premia ilisema Ijumaa.

Kumekuwepo na uvumi kwenye vyombo vya habari kwamba angeondoka lakini baada ya madifenda wawili wenye uzoefu, Nemanja Vidic na Rio Ferdinand, tayari wakiwa njiani kuondoka, United walikuwa na “furaha isiyo na kifani” kutangaza kwenye tovuti yao kwamba Evra atasalia katika klabu hiyo.

Mfaransa huyo aliyetimiza umri wa miaka 33 wiki iliyopita, alijiunga na United kutoka AS Monaco mwaka 2006 na amewachezea mara 379, na kushinda mataji 10 makuu.


Amekuwa beki wa kushoto nambari wani na amekuwa akishikilia wadhiwa wa nahodha Vidic akiwa hayuko mara nyingi.

Mholanzi Alex Buttner alitua Old Trafford mwaka 2012 kuwa msaidizi wa Evra na vyombo vya habari Uingereza vinasema United wamewasilisha ofa ya £27 milioni kununua difenda wa miaka 18 wa Southampton Luke Shaw kujaza nafasi hiyo kwa siku za baadaye.

United wanatarajiwa kufanyia kikosi chao mabadiliko makubwa kabla ya msimu ujao chini ya meneja wao mpya Louis van Gaal baada ya kumaliza nambari saba kwenye Ligi ya Premia mwaka mmoja tu baada yao kutwaa ubingwa mara ya 20 Uingereza.