come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

MAKALA: KUTOKA BAD GEAR HADI WITNESS MWAIJAGA

Na Robert Michael 0752 711688

Namfahamu tangia akiwa anasota kwenye gemu kitambo sana, alikuwa akifahamika sana kwa jina la Bad Gear na miongoni kati ya wasanii wa kwanza kwa upande wa akina dada.


Enzi hizo wanamuziki wengi wa kiume ambapo walikuwa wakitembea kwa miguu kutoka majumbani kwao kuelekea studio, nakumbuka studio zilikuwa chache ambazo ni pamoja na Don

Bosco iliyokuwa chini yake Bonny Luv na Sound Crafters.Hapo ndipo mwanadada Bad Gear alipoanza harakati zake za kuimba hiphop, alishangaza sana kwa uwezo wake na jinsi alivyokuwa akiumuiga mwanadada hatari kwa kurap tokea nchini Marekani MC Lyte.

Bad Gear alikumbana na skendo mbalimbali kuhusishwa na tabia yake ya ubabe kutokana na kujaaliwa mwili mkubwa pia alihusishwa na kuwa na uhusiano wa mapenzi na mwanahip hop mwenzake wakati huo Crazy Buffa.

Lakini aliendelea kutafuta maisha kupitia muziki ambapo alishindwa kutoka, nakumbuka wakati huo ukumbi wa Amana Vijana Centre uliopo Ilala jijini Dar es Salaam ulikuwa na matamasha yake ya muziki wa hiphop kila siku ya Ijumaa.

Bad Gear alisota kila kona kutafuta mafanikio lakini wapi! hakufanikiwa kutoka zaidi zaidi akina dada Zay B na mwenzake Sista P walipata mafanikio makubwa huku yeye akiishia kusikojulikana.

Lakini mipango si matumizi, Bad Geara alijipanga vema na kusikiliza maneno ya washauri wake ambapo aliamua kurejea upya kwenye gemu, lakini safari hiyo sasa alibadili jina lake la Bad Gear na kutumia jina lake halisi.

Aliibukia kwenye kundi la Wakilisha lilikouwa na nyota watatu Langa (Marehemu) na Shaa, kundi hilo lilitamba katika shindano la kusaka vipaji liliokuwa likiendeshwa kama Bongo Stars Search.

Cocacola star search liliofanyia nchini Kenya, kundi hilo liliweza kutamba hapa nchini na kufanikiwa kupendwa, ndipo umaarufu wa mwanadada huyo ulipoongezeka.

Witness alijulikana kioa kona ya nchi kutokana na uwezo wake wa kurap na kufanikiwa kutunga na kuimba nyimbo mbalimbali, hata hivyo kundi hilo lilimeguka ambapo kiola msanii aliamua kufanya shughuri ya muziki kivyake.

Ndipo Witness alipoamua kutoa wimbo wake uliokuja kubamba uitwao 'Ziro' baadaye akaja na mwingine 'Attention', mwanadada huyo anayetokea Tukuyu mkoani Mbeya amefanya ziara nyingi barani Ulaya na hivi karibuni alitembelea Marekani.