|
|
Mfungaji mabao bora wa Real Madrid Cristiano
Ronaldo yuko sawa kucheza fainali ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya Jumamosi
dhidi ya Atletico Madrid lakini bado kuna shaka kuhusu fowadi Karim
Benzema na mkabaji wa kati Pepe, kocha Carlo Ancelotti alisema Ijumaa.
Ronaldo, ambaye amefunga mabao 16 msimu huu katika dimba hilo kuu la klabu Ulaya, amekuwa akisumbuliwa na majeraha ya misuli wiki za majuzi na hajacheza tangu achechemee kutoka wka mechi ya La Liga dhidi ya Real Valladolid Mei 7.
Benzema naye alijeruhiwa misuli ya paja wakati wa ushindi wao wa 3-1 Jumamosi nyumbani dhidi ya Espanyol, huku Pepe naye akiwa amekaa nje tangu ajeruhiwe misuli ya sehemu ya chini ya mguu wakati wa mechi hiyo ya Valladolid
.
"Cristiano yuko sawa, alifanya mazoezi vyema,” Ancelotti aliambia kikao cha wanahabari kabla ya kikao cha mwisho cha mazoezi cha Real kabla ya kivumbi katika uwanja wa Stadium of Light wa Benfica mjini Lisbon.
“Lazima tuchunguze zaidi hali ya Pepe na Benzema kwa sababu hawajafanya mazoezi wiki hii,” aliongeza Mwitaliano huyo, ambaye anapigana kuwa kocha wa pili baada ya Bob Paisley wa Liverpool kushinda Kombe hilo la Ulaya mara tatu.
"Baada ya kikao cha mazoezi usiku wa leo tutafanya uamuzi kuhusu mechi hiyo ya kesho.”
Ancelotti anaweza kutumia Alvaro Morata nafasi ya Benzema, naye Raphael Varane ambaye kawaida husaidia Pepe ajaze nafasi yake, au kama wote wawili hawatakuwa, basi mkabaji wa kati Sergio Ramos anaweza kutumiwa.
Kocha huyo hata hivyo ataumizwa kichwa na safu ya kati, ambapo anahitaji kuamua nani atajaza nafasi ya Xabi Alonso ambaye amesimamishwa kucheza.
Ufanisi wa Real msimu huu kwa kiwango kikubwa umechangiwa na Alonso wa Uhispania ambaye huwafaa kwa ujuzi wake wa kusambaza mpira na kukabili wapinzani.
Asier Illarramendi, aliyekosa kupendeza msimu wake wa kwanza, au Sami Khedira, aliyerudi tu majuzi baada ya kufanyiwa upasuaji kwenye goti, ndio wachezaji wawili pekee wanaoweza kujaza nafasi yake.
USIKU MMOJA
"Nina usiku mmoja zaidi wa kutafakari kuhusu hilo na kesho nitafanya uamuzi,” alisema Ancelotti, aliyeshinda Kombe hilo la Ulaya na AC Milan mara mbili akiwa kama mchezaji na mbili akiwa kocha.
Aliongeza kwamba “ndoto” yake ni kuona uchezaji karibu sawa na waliocheza kwenye mechi ya marudiano ya nusufainali wakiwa Bayern Munich, ambapo Real waliaibisha mabingwa hao watetezi 4-0 katika Allianz Arena na kusonga mbele 5-0 kwa jumla.
“Tukicheza tulivyofanya dhidi ya Bayern tuna nafasi,” akasema Ancelotti.
"Mengi hupitia katika kichwa chako kabla ya mechi kama hii. La muhimu zaidi ni kutulia, kufanya mazoezi vyema, na kudhibiti mambo na kutoa maagizo mema kwa timu.
“Badala ya kufikiria kuhusu hotuba za kabla ya mechi, mimi huangazia zaidi mbinu na maagizo ya kuwapa wachezaji, jinsi ya kusakata mechi.”