come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

RONALDINHO AJA NA MPYA BAADA YA KUTEMWA KIKOSINI

BAADA ya kutemwa kwenye kikosi cha kocha Luiz Felipe Scolari cha Brazil kitakachoshiriki Kombe la Dunia, Ronaldinho ameibuka na mengine ya kutengeneza fedha kupitia michuano ya mwaka huu.


Mshambuliaji huyo wa zamani wa Barcelona ameamua kupangisha jumbo lake la kifahari liliopo Rio de Janeiro kwa gharama za Pauni 9,120 kwa siku, ili kuwapa mashabiki fursa ya kuishi kwenye mjengo wa kifahari wa gwiji huyo wa Brazil.

Ronaldinho ameposti kwenye Twitter kuthibitisha kwamba jumba lake lenye vyumba vitano vya kulala linapangishwa kupitia Airbnb.com wakati wa Kombe la Dunia mwaka huu.

Nyota huyo wa Atletico Mineiro ameandika: "Hii ni kwa yeyote ambaye anaona anaweza kupanga nyumba yangu Airbnb! jiachie katika mjengo wa #CasaR10'Ronaldinho's property, ambao pia una vyumba sita vya kulala, upo ndani ya geti mjini Rio eneo la Barra da Tijuca.

Yeyote anayeweza kupanga katika mjengo huo wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34 ague kwamba una kitu ikiwemo sauna, barbeue, a cellar na friji la bia.

Ronaldinho aliyechezea pia PSG na AC Milan, amelipendezesha jumba hilo kwa kuweka michoro ya picha zake mbalimbali na mtu anayetaka kupanga anatakiwa kutoa malipo ya awali ya Pauni 600, lakini hairuhusiwi kuvuta sigara ndani, labda nje ya nyumba na kutakuwa na timu maalum ya watu wa kuhudumia wageni.