come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

AKAUNTI YA FACEBOOK YA MUIGIZAJI BABA HAJI YAVAMIWA NA MATAPELI

Staa wa filamu nchini Haji Adam "Baba Haji" amepatwa na masahibu baada ya akaunti yake ya Facebook kuwa hacked na matapeli ambao pia wanapost vitu vya kumchafua na kumdhalilisha.

Kwa mujibu wa mtu wa karibu na Baba Haji akizungumza na Mikito ya Anko Matua amesema kuwa matapeli hao walianza kwa kuandika post chafu za ushoga na kujifanya wao ni Baba Haji na sasa wameanza kupost kuhusu Zito Kabwe Foundation ili kuwatapeli watu ambao watadhani ni baba haji kweli ndiye amepost.

Juhudi zinafanyika kuirudisha akaunti yake kama mwanzo.Angalizo: Watu maarufu na hata watu wa kawaida wenye likes nyingi na marafiki wengi facebook ndiyo huwa wahanga wakubwa wa tatizo hili kwa kuwa siku zote hackers huwa-target watu wengi ili kufanikisha mambo yao kirahisi.

Ukitumia link na mtu usiyemjua akikushawishi uifungue usiifungue kwasababu ukiifungua link hiyo inatafsiri moja kwa moja email na pasword yako na wao kuingia na kuichezea akaunt au page yako watakavyo.


Wakati mwingine wanaweza kukutumia link na kukuambia tumeona picha zako chafu sehemu flani funguo hiyo link uangalie na wewe kwa mshangao wa kutaka kuona hizo picha chafu zinazodaiwa kuwa zako ukiifungua umekwisha kwasababu hutakuta picha zako chafu wala nini bali ni link ya ku-hack akaunt yako.