Uongozi wa timu ya soka ya Mtibwa Sugar ya Turiani mkoa Morogoro imesema klabu ya Simba imekiuka taratibu za usajili na wako tayari kuishitaki TFF, Akizungumza jana msemaji wa timu hiyo Thobias Kifaru amesema kuwa Simba imefanya usajili wa kumchukua kipa wake Hussein Sharrif 'Cassials' wakati bado ana mkataba na timu yao.
Kifaru amedai kwamba mpaka sasa viongozi wa Mtibwa hawajakutana kuzungumzia suala hilo kufuatia msiba wa mlezi wao, ameongeza kuwa lazima sheria ifuate mkondo wake kwani Cassilas ni mchezaji wao kisheria na ana mkataba wa mwaka mmoja hivyo ni ngumu kusajiliwa na timu nyingine pasipo kuzungumza na uongozi kwanza.
'Simba imekosea ilibidi waje huku Manungu kuzungumza na sisi najua tungekubaliana tu kwani Cassilas ni mali yetu na amebakiza mwaka mmoja, hivyo kwa kumsajili na kumtangaza kuwa ni mali yao tunakwenda TFF kupeleka malalamiko yetu na ikibidi Simba iadhibiwe.
Jana uongozi wa klabu ya Simba ulimnadi kipa bora wa ligi kuu bara Hussein Sharrif 'Cassilas' kwenye vyombo vya habari na kusema ni mali yao na tayari wamempa mkataba wa miaka miwili