come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

TETESI ZA USAJILI MAJUU

Chelsea wako tayari kumuuza John Obi Mikel kwa pauni milioni 5 na klabu kadhaa za Serie A za Italia zimeambiwa zinaweza kumchukua (Daily Mail).


Meneja wa Manchester City, Manuel Pellegrini amekataa kuzungumza na Chama cha Soka cha Brazil kuhusu kuchukua nafasi ya Luiz Filipe Scolari kuifundisha timu ya taifa (El Mercurio).

Real Madrid wamekubaliana na James Rodriguez. Real Madrid wana subiri kukubaliana na Monaco wanaotaka ada ya uhamisho kuwa euro milioni 80 (AS) West Ham watakamilisha usajili wa Enner Valencia siku ya Jumatano kwa mkataba wa euro milioni 15 (Daily Mail)

Swansea wamekataa pauni milioni 8 zilizotolewa na Liverpool kumsajili Ben Davis (Daily Telegraph), Manchester United, Chelsea na Arsenal watatakiwa kutoa zaidi ya euro milioni 75 ili kumsajili mshambuliaji wa Paris St-Germain, Edison Cavani (talkSPORT)

Everton wanakaribia kukamilisha usajili wa kiungo wa Fevencvaros Muhamed Besic kwa pauni milioni 4 (Daily Mail), Trabzonspor ya Uturuki wanamfuatilia beki wa Liverpool Kolo Toute (Daily Mail)

Newcastle wanakaribia kukamilisha usajili wa Emmanuel Rivière kutoka Monaco (Daily Mail), hatua ya Manchester United kumtaka Arturo Vidal kwa pauni milioni 35 kumesababisha boss wa Juventus kujiuzulu kwa hasira (The Sun)

Besitkas wanamtaka Demba Ba, 29, kwa mkopo huku wakitaka kufanya uhamisho huo kuwa wa kudumu baada ya msimu (Daily Mirror), AC Milan wanamtaka winga wa Manchester United Nani (Football Italia)

Manchester United wanawafuatilia kwa makini kuwapa majaribio Joao Virginia, 15, aliyepewa jina la 'Cristiano Ronaldo mpya' na kipa Joao Virginia, 15, kutoka Porto (Skysports)