Yanga imesema itashiriki michuano hiyo ya kila mwaka, baadaye mwezi ujao, endapo itaarifiwa rasmi na Shirikisho la Soka la Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) ambao ndiyo waandaaji.
Akizungumza jana, Afisa Habari wa Yanga, Baraka Kizuguto alisema uongozi haujatangaza kokote kwamba Yanga haitakwenda Rwanda, isipokuwa imekuwa ikisema haina taarifa zozote juu ya ushiriki.
Kizuguto alisema Yanga haina sababu ya kutoshiriki michuano hiyo, lakini ni vigumu kusema lolote wakati haina taarifa zozote kutoka CECAFA.
"Bado hatujapata taarifa zozote na hatujatoa msimamo juu ya ushiriki wetu, hizo taarifa kwamba sisi hatuendi zinatoka wapi?" aliuliza Kizuguto.
"Subiri CECAFA watuletee taarifa za kimaandishi muone kama Yanga itakwenda Kagame au haiendi.
"Yanga haina haja ya kuwa na hofu juu ya michuano hiyo kwa sababu ina kikosi imara na kocha bora (Marcio Maximo)."
Makocha wa Yanga: kikosi kipo tayari kwa kushiriki kagame
Hata hivyo kauli ya Kizuguto inatofautiana na taarifa za Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka (TFF) kuwa, Selestine Mwesigwa kwamba Yanga inazo taarifa juu ya michuano hiyo kwa sababu amekuwa akiwasiliana nayo.
"TFF ni TFF na Yanga ni Yanga. Ukweli ni kwamba hatuwezi kuwa watoto wadogo kuongopa hakuna taarifa wakati tunazo," alisema Kizuguto na kueleza zaidi, "uongozi haujafahamishwa na ndivyo hali ilivyo.
"Ila kuhusu ushiriki au kutoshiriki hatujaamua kwa vile hatuna taarifa rasmi sasa tutaamuaje?"
Yanga iliyotwaa ubingwa wa Kagame mara mbili mfululizo mwaka 2011 na 2012 kati ya jumla ya mataji matano iliyonayo, ilishindwa kwenda kujitetea mwaka jana michuano ilipofanyikia Sudan Kaskazini kwa hofu ya usalama.