come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

CHELSEA YAPIGWA 3-0 MBELE YA DROGBA

Didier Drogba 

Chelsea walilishwa kichapo chao cha kwanza katika mechi za kujiandaa kwa msimu Jumapili walipolazwa 3-0 na Werder Bremennchini Ujerumani na kuharibu kurudi kwa Didier Drogba na pia kuanza mechi kwa kipa Thibaut Courtois.

Kigogo wa Ivory Coast Drogba alichezea Chelsea mara ya kwanza tangu afunge penalti iliyowashindia Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya mjini Munich alipoingia kama nguvu mpya kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Diego Costa aliyenunuliwa majira haya ya joto.

Hata hivyo, vijana hao wa Jose Mourinho walikuwa tayari 2-0 chini wakati huo na kurudi kwa Drogba kuliishia kichapo uwanjani Weserstadion.

Nahodha wa The Blues John Terry alisababisha penalti nyepesi baada ya dakika 20 za mchezo alipotumia mkono kuzuia mpira na winga Mholanzi Eljero Elia akambwaga kipa Mbelgiji Courtois, aliyejiunga na Chelsea baada ya kukaa kwa muda mrefu kwa mkopo Atletico Madrid.


Mambo yalizidi kuwa mabaya kwa wageni dakika 17 baadaye Terry alipoadhibiwa tena na winga wa Poland Ludovic Obraniak akabwaga Courtois kwa kichwa.
Mourinho alifanya mabadiliko kadha, ikiwemo kuingiza Drogba na Branislav Ivanovic, huku Eden Hazard naye akiingia mchezoni kipindi cha pili.

Bremen walipata penalti ya pili dakika ya mwisho pale difenda wa Uholanzi Nathan Ake alipoadhibiwa kwa kile kilichoonekana kuwa kumkabili mpinzani vyema, lakini hilo halikumjalisha Felix Kroos, aliyembwaga kipa nguvu mpya Petr Cech kutoka hatua 12.

Chelsea, ambao awali walikuwa wameshinda mara nne na kutoka sare moja mechi zao za kujiandaa kwa ligi, wataendelea na maandalizi yao kwa mechi dhidi ya Ferencvaros ya Hungary mjini Budapest Jumapili ijayo.