come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

GLAZERS KUPATA $150 MILIONI KWA KUPUNGUZA HISA MAN UNITED

Wayne Rooney

Familia ya Glazer itatengeneza $150 milioni kwa kuuza sehemu ya hisa zake Manchester United ingawa uuzaji huo bado utaacha Wamarekani hado wakwia bado wanadhibiti klabu hiyo ya soka ya Uingereza.

Glazers, walionunua United £790 milioni 2005, wanauza hisa milioni nane kati ya hisa wanazomiliki katika klabu hiyo ambazo ni sawa na asilimia tano.
Hisa hizo zikiuzwa, watoto sita wa marehemu Malcolm Glazer bado watamiliki zaidi ya asilimia 80 ya hisa zote za klabu hiyo.

Mapato yote ya uuzaji huyo hayataenda kwa klabu hiyo, jambo ambalo huenda likaudhi baadhi ya mashabiki ambao wamepinga wamiliki hao ambao wanawashutumu kwa kulimbikizia United madeni tangu wachukue umiliki.


Kuuzwa kwa hisa hizo kutaongeza hisa za United sokoni baada ya kuanza kuuzwa kwa hisa hizo Soko la Hisa la New York miaka miwili iliyopita.
Hisa hizo zilianza kuuzwa $14 na bei imepanda hadi kufikia $19.31 Jumatano, na kufanya thamani ya klabu hiyo kuwa takriban $3.2 bilioni.

United, wanaoshikilia rekodi ya kushinda ligi ya soka Uingereza wakiwa wameshinda mara 20, wanapanga kujikwamua baada ya msimu mbaya ambao walimaliza nambari saba katika Ligi ya Premia na kukosa kufuzu kwa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.

Matumaini yamefufuliwa na kuwasili kwa meneja mpya, Mholanzi Louis van Gaal, na kutiwa saini kwa mkataba mpya wa vifaa vya michezo na Adidas wa thamani ya £750 milioni kwa miaka zaidi ya 10. General Motors Co walitia saini mkataba wa $559 milioni wa udhamini wa miaka saba wa klabu hiyo kupitia nembo ya GM ya magari ya Chevrolet, ambayo itakuwa kwenye jezi za timu.

Glazers pia humilki timu ya NFL ya The Tampa Bay Buccaneers. Mkuu wa familia hiyo Malcolm Glazer alifariki mapema mwaka huu.

Wasimamizi wa uuzaji wa hisa hizo ni Jefferies, BofA Merrill Lynch, Credit Suisse, Deutsche Bank na Nom.