|
|
Mshikiliaji rekodi ya mabao mengi zaidi katika
Kombe la Dunia na straika mkongwe wa Ujerumani, Miroslav Klose, hatimaye
amestaafu kutoka kandanda ya kimataifa huku wengi walituma risala za
pongezi Jumatatu.
Klose, alipatia Ujerumani mkono wa buriani kama bingwa wa dunia pale aliposaidia kikosi cha kocha Joachim Leow kunyakua Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza tangu 1990 walipolaza Argentina 1-0 kwenye fainali iliyochezwa Rio de Janeiro, Brazil.
Klose alitia kizimbani bao lake la 15 na 16 na kupita rekodi ya zamani ya nyota mstaafu wa Brazil, Ronaldo, huku akishiriki kombe lake la nne la dunia.
Klose, ambaye alishinda mataji mawili ya Bundesliga na Bayern Munich baada ya kuchezea Kaiserslautern na Werder Bremen, alisema kwenye taarifa ya kustaafu kwake iliyotolowe na shirikisho la kandanda Ujerumani kuwa “nimetimiza ndoto ya utotoni kwa kushinda taji la dunia Brazil,” na “sitosahau muda wangu na kikosi cha taifa.”
“Ufanisi wa timu ndio nguzo kubwa zaidi kwangu na tuliweza kutimiza lengo kuu pamoja kama kikosi.”
“Nilitimiza malengo ya kibinafsi na wanao nifahamu wanajua kuwa nina malengo makubwa zaidi lakini kama mshambuliaji, jukumu kubwa ni kufunga magoli.
“Rekodi hazikunitia wasiwasi lakini langu lilikuwa kujitolea kabisa kusaidia kikosi.”
Klose, alizaliwa Poland, alitia kizimbani mabao matano kwenye shindano la 2002 lakini taifa lake likazamishwa 2-0 na Brazil kwenye fainali ambao Ronaldo alifunga magoli yote.
Aliongezea matano zaidi wakati Ujerumani waliandaa Kombe la Dunia la 2006, mane Afrika Kusini 2010 na mawili Brazil kutwaa uongozi katika shindano hilo.
Pele na Mjerumani mwenzake Uwe Seeler ndio wachezaji wengine pekee kuwahi funga magoli kwenye awamu nne za dimba hilo na anaondoka jukwaani akiwa kiongozi wa Ujerumani kwenye historia akiwa na magoli 71 katika mechi 137.
“Ilikuwa ni heshima kuu kwa Miro kuitwa kwenye kikosi cha taifa. Alitia bidii yake yote kwa Ujerumani,” Leow alisema kwenye risala za sifa zilizofuata tangazo hilo.
“Ninaheshimu pakubwa uamuzi wake na kwa kufanikiwa zaidi na timu ya taifa. Itakuwa vigumu kwa yeyote mwingine kupita kiwango chake,” aliongeza.
Rais wa shirikisho, Wolfgang Niersbach, naye alitangaza, “Klose si mchezaji wa aina yake pekee wala ni mwanaume kielelezo.”
“Ameanidikisha rekodi mbili, ya Ujerumani na Kombe la Dunia ambazo zitahakikisha sifa zake zimepata mahala pa heshima katika historia.”
“Asante Miro. Takwimu zako zazungumza zenyewe lakini umaahiri wako unadhihirika zaidi kama binadamu,” Mario Goetze, ambaye alifunga bao la ushindi kwenye fainali ya Kombe la Dunia, aliandika kwenye anwani yake ya Twitter.