Kocha wa Manchester City
Manuel Pellegrini amesema anamatumaini makubwa timu hiyo italitetea taji
lake licha ya kuambulia kichapo cha mabao matatu kwa nunge dhidi ya
vibonde wao Arsenal katika mechi ya kuwania ngao ya Community hapo jana.
Man City, wameratibiwa kufungua kampeini ya kutetea taji lao dhidi ya Newcastle jumapili ijayo.
Baada ya kichapo hicho hiyo jana
Pellegrini aliulizwa na BBC Michezo iwapo anamatumaini kuwa timu hiyo
inauwezo wa kutetea taji lake Pellegrini alisema kwa kinywa kipana
ndiyo.
'' Nafahamu kuwa msimu huu timu 5 au hata 6
zinauwezo wa kutwaa taji la ligi msimu huu lakini nakuhakikishia kuwa
kati ya timu hizo zote Man city ndiyo inatimu yenye uwezo wa kushinda.''
alisema Pellegrini.
''Wajua ni vigumu kuamini lakini mkitupa muda tutawathibitishia hilo uwanjani''.
Man City iliambulia kichapo cha 3-0 dhidi ya Arsenal.
Pellegrini alisema kutokuwepo kwa mshambulizi
wake machachari Sergio Aguero mlinzi Vincent Kompany, Pablo Zabaleta
na Bacary Sagna liathiri mchezo wetu.
''Unafahamu kuwa kikosi kilichocheza hivi leo sio kikosi chetu cha kwanza ''.
Pellegrini alimpa nafasi ya kuanza mchezaji mpya
Willy Caballeroin na akamwelezea kipa nambari moja msimu uliopita Joe
Hart, kuwa lazima adhihirishe uwezo wake msimu huu kwani anaupinzani si
haba.