come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

MSIBA MZITO YANGA SC

DEREVA wa basi la Yanga SC, Maulid Kiula amefariki dunia asubuhi ya leo nyumbani kwake, Dar es Salaam.

Meneja wa Yanga SC, Hafidh Saleh ametoa taarifa za awali za msiba wa marehemu na taarifa zaidi zitatolewa baadaye.
Mau ni mwana Yanga wa siku nyingi ambaye amekuwa akijitolea kufanya kazi za klabu tangu ikiwa haiko vizuri kiuchumi.
Pumzika kwa amani Maulid Kiula

Amepitia changamoto nyingi akiwa kazini Yanga SC, ikiwemo kupata ajali na kushambuliwa kwa mawe na mashabiki wa timu pinzani.

Huyu ndiye dereva ambaye alikuwa anaendesha basi la Yanga SC wakati likishambuliwa kwa mawe na mashabiki wa Mbeya City mwaka jana mjini Mbeya.


Na huyu pia ndiye dereva aliyekuwa anaendesha basi la Yanga SC wakati likiacha njia na kukaribia kupinduka, timu ikitokea Morogoro mwaka huu, lakini kwa umahiri wake gari halikupinduka.

Msiba wa Mau si pigo kwa Yanga SC tu, bali kwa familia yake zake zaidi, ambayo ilikuwa inamtegemea kwa kila kitu. Mungu ampumzishe kwa amani kijana huyo mpole, muadilifu na muungwana. Mungu aijaalie subira familia yake katika wakati huu mgumu kwao. Amin