|
|
Mshambuliaji mpya wa Arsenal, Danny Welbeck,
alizamisha magoli yote mawili na kuwezesha Uingereza kuandikisha ushindi
wa 2-0 ugenini Uswisi na kuzindua kampeni yao ya kufuzu Kombe la Ulaya
la 2016 kwa msisimuko mkubwa.
Mechi hiyo iliyochezwa Basel ilishuhudia Uingereza ambao wamekashifiwa nyumbani kwa utepetevu baada ya matokeo mabaya katika Kombe la Dunia yaliofuatiwa na uzembe dhidi ya Norway kwenye mechi ya kujipima nguvu, wakidhibiti mchezo kwa vipindi virefu.
Bao lao la kwanza liliwasili katika dakika ya 58 ya kipindi cha pili wakati Welbeck alipomaliza shambulizi la haraka la mshtuko lililohusisha nahodha wake Wayne Rooney na Raheen Sterling.
Uingereza waliopeteza nafasi mingi za kufunga walihakikishia ushindi wakati Welbeck alipotia kizimbani lake na lao la pili katika dakika ya kikomo ya muda wa kawaida kwenye uga wa St Jakob-Park.
“Dhamira yetu ilikuwa kuanza kwa kishindo na kuendeleza mtindo huo hadi mwisho na mwishowe, tulipata zawadi tuliostahili. Tulilazimisha mchezo lakini bao la kwanza lilihitajika ilikuwashawishi watushambulie na kupata nafasi za kuliongezea,” meneja wa Uingereza, Roy Hodgson, alisema.