|
|
Kiungo wa Chelsea, Cesc Fabregas, amekiri kuwa
waajiri wake wa zamani, Arsenal watasalia moyoni mwake milele lakini
azima yake sasa ni kusaidia klabu chake kipya kushinda mataji.
Fabregas alitumikia miaka minane Arsenal alipopanda ngazi hadi kuwa nahodha na kuwachezea zaidi ya mechi 300 kabla ya kusaini na Barcelona alipokaa miaka mitatu na kuhamia Chelsea hivi majuzi.
Arsenal walikuwa na chaguo la kwanza kumsaini tena lakini wakakataa na Fabregas alielekea kwa waasimu wao Chelsea kwa ada ya pauni milioni 30.
Chelsea watakaribisha Arsenal Oktoba 5 kwenye uga wao wa Stamford Bridge kwenye mechi ya ligi ya Premier na ingawa Fabregas anakubali klabu chake cha zamani bado ni spesheli kwake, amesisitiza hilo halitomuadhiri.
“Nitadumisha hisia za Gunners milele na ninajua nitarudi Emirates na itakuwa ni muda wa kipekee lakini zaima yangu ni kusaidia Chelsea sasa,” Fabregas alisema.