Muimbaji Chris Brown amejikuta aki ‘spend’ weekend yake akiwa katika hali ya wasiwasi baada ya kupata vitisho vya kumuondoa uhai kutoka kwa watu wasiofahamika.
Kwa mujibu wa vyanzo, mwanasheria wa Chris, Mark Geragos
alipokea simu kutoka kwa watu tofauti wasiojulikana
wakitishia kumuua Chris Brown bila kutoa sababu. Baada
ya vitisho hivyo Geragos aliamua kutoa taarifa idara ya
polisi ya Los Angeles ambao wanaendelea kufanya upelelezi
juu ya vitisho hivyo.
Hivi karibuni Chris Brown amekosa maelewano mazuri na
majirani zake kutokana na wao kutofurahishwa na graffiti ya
Chris aliyoichora nje ya uzio ya nyumba yake ya Hollywood
Hills kwa madai kwamba kuna watoto wadogo ambao wanaishi
na kupita eneo hilo ambao wanatishika na michoro hiyo yenye muonekano unaotisha, kitu ambacho kinahisiwa kuwa kinaweza kuwa
moja ya sababu za vitisho alivyovipata.
|