Washindi wa kombe la Uropa mwaka
wa 2015 watafuzu moja kwa moja kwa michuano ya kuwania kombe la klabu
bingwa barani Ulaya msimu utakaofuata.
Hayo yamethibitishwa rasmi na shirikisho la mchezo wa soka barani Ulaya EUAFA.
Kwa mujubi wa UEFA, umauzi huo umechukuliwa ili kuimarisha viwango vya soka katika fainali hizo na pia kuifanya ligi hiyo ya Uropa ambayo ni ya pili kwa ukubwa kuvutia zaidi.
Uamuzi huo uliochukuliwa wakati wa mkutano mkuu wa EUFA, inajiri baada ya miezi kadhaa ya mazungumzo kati cha shirikisho hilo na chama kinachoakilisha vilabu barani Ulaya..
Wakati huo huo mkutano huo, umeidhinisha kuwa fainali ya kombe la klabu bingwa barani Ulaya mwaka wa 2015, itachezwa katika uwanja wa Olimpiki wa Berlin, huku fainali ya kombe la Uropa kuchezwa katika uwanja wa Kitaifa wa Warsaw.
Ligi ya Uropa haizalishi kiasi kikubwa cha fedha na pia haiangaziwi pakubwa na vyombo vya habari kwa michuano ya klabu bingwa barani Ulaya.
Kwa mara kadhaa EUFA imejaribu mikakati kadhaa ya kuifanya shindano hilo kuvutia zaidi ikiwemo kubadili jina kutoka kwa kombe la UEFA mwaka wa 2009 na kuitwa kombe la Uropa.
Kwa sasa, timu zinazomaliza katika nafasi ya tatu katika makundi yao kwenye fainali za klabu bingwa hushushwa daraja na kushiriki katika kombe hilo la Uropa.
Fainali ya mwaka huu, ilivutia timu mbili ambazo zilifuzu kuambatana na sheria hiyo, na Chelsea ikiibuka na ushindi wa magoli mawili kwa moja dhidi ya Benfica katika fainali.