KLABU ya Chelsea imeonyesha nia ya
kumsajili winga wa kimataifa wa Uturuki, Arda Turan, ambaye kwa sasa
anachezea Atletico Madrid.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26,
ameivutia klabu yake ya zamani, Galatasaray lakini rais wake, Unai Aysal
amesema wanakabiliwa na upinzani kutoka Stamford Bridge.
Alisema: "Chelsea wamo kwenye mbio za kumsajili Arda na hatutakuwa tayari kushindana na ofa watakayotoa.
"Nimekutana na kiongozi wa Atletico
Madrid, ameniambia kwamba kulikuwa kuna wachezaji watatu hawataki
kuwauza, mmoja wao ni Arda Turan.'
Wakati huo huo, Atletico ni miongoni mwa
klabu ambazo zinammezea mate kiungo wa QPR, Esteban Granero. Mchezaji
huyo mwenye umri wa miaka 25, pia anatakiwa na Fulham, Sevilla na Real
Betis.
Na Manchester City iko tayari kumtoa kwa
mkopo mshambuliaji wa Hispania, Dennis Suarez kwenda Sevilla, Granada
na Espanyol wanaomuhitaji mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 19.