KAULI ya mwenyekiti wa kamati ya usajili ya klabu ya Simba Zackaria Hanspope kwamba Yanga imeingizwa mjini kuhusu usajili wa kiungo mshambuliaji Mrisho Ngassa ambaye jana alitambulishwa mbele ya waandishi wa habari kwamba ametua rasmi katika klabu yake anayoipenda.
Hanspope alijibu mapigo na kudai usajili wa Ngassa ni sawa na kuingizwa mjini na ameitaka Yanga kuilipa Simba shilingi Milioni 50 ama sivyo watalishupalia suala hilo mpaka TFF.
Kauli ya Hanspope imeonyesha kuishiwa maneno na kujuta kwanini alirejea Simba kwani Yanga imemsajili Ngassa akiwa mchezaji huru baada ya mkataba wake na Azam kumalizika mwezi huu, Akizungumza huku akijiamini msema ji wa Yanga Baraka Kizuguto amesema kwamba kauli ya Hanspope haina mashiko kwa wanamichezo.
Ngassa ni mchezaji huru na makataba wake unaotambuliwa na TFF ni ule wa Azam ambao walimpeleka Simba kwa mkopo, Hivyo Simba ndio wameingizwa mjini na si Yanga, Ngassa jana alitambulishwa kwa waamndishi wa habari baada ya kusaini Yanga kwa mkataba wa miaka miwili.
Pia amekabidhiwa gari la kifahari aina ya Nissan, Akizungumza huku akiwa na furaha, Ngassa alisema kwamba amefurtahi kurejea katika klabu yake anayoipenda ya Yanga, Ila akiwa kama mchezaji ni wajibu wake kucheza kwa bidii akiwa timu nyingine zaidi ya Yanga