
Diamond Platnumz
Akizungumzia tamasha hilo jana jijini Dar es Salaam, Meneja wa Chapa ya Tigo, William Mpinga, alisema lengo la tamasha hilo ni kuwapa burudani mashabiki wa muziki jijini Mwanza na pia kujenga mahusiano ya karibu na wananchi kupitia sanaa ya muziki.
Mpinga aliwataja wasanii wengine nyota watakaokuwapo katika tamasha hilo kuwa ni Madee wa Tip Top Connection, Ney Wamitego, Roma Mkatoliki, Rich Mavoko, Recho, Kazi Kwanza na Fid Q.
Akizungumzia tamasha hilo, Diamond alisema kuwa yeye na wenzake wanafurahia tamasha hilo la wazi la Tigo kwani litawapa nafasi ya kuwakutanisha na mashabiki wao wa jiji la Mwanza.
“Nina furaha ya kipekee kufanya tamasha kubwa la wazi jijini Mwanza, naamini mashabiki wangu waliokuwa wakitamani kuniona lakini wakishindwa kutokana na viingilio vya kwenye kumbi, sasa watapata nafasi kupitia tamasha hili la Tigo,” alisema Diamond.