come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

Matatu ya Oduamadi yazamisha Tahiti

Nnamdi Oduamadi

Nnamdi Oduamadi alifunga mabao matatu huku Nigeria ikipuuzilia mbali hofu ya uchovu wa safari ya ndege na kuadhibu wanyonge Tahiti 6-1 katika mechi yao ya kwanza Kombe la Confederations mjini Belo Horizonte mnamo Jumatatu.

Mabingwa hao wa Afrika waliwasili Brazil saa 36 pekee kabla ya mechi baada ya mzozo kuhusu malipo ya bonasi, lakini waliweza hata kupoteza nafasi nyingi za kufunga na kuwaruka mabingwa wa dunia Uhispania hadi kileleni mwa Kundi B.
Ilikuwa ni mechi ya uchungu mwingi uliosubiriwa kwa Tahiti ambao wamo nambari 138 orodha ya soka duniani, lakini waliweza kushangilia baada ya Jonathan Tehau kufunga kwa kichwa bao lao la kwanza kabisa kuwahi kufungwa na timu hiyo dimba kuu la kimataifa.
Bao la Tehau, dakika za kwanza za kipindi cha pili, lilipunguza uongozi wa Nigeria hadi 3-1 baada ya mpira uliotoka kwa Uwa Echiejile kugonga mchezaji na kuingia ndani na mabao mawili ya Oduamadi kukabidhi Nigeria udhibiti wa mechi.
Hata hivyo, matumaini ya wakazi hao wa kisiwa kilichoko Pacific kusini kujikwamua yaliyeyuka baada ya Tehau kujifunga mwenyewe kabla ya Oduamadi na Echiejile kuongeza magoli mengine na kuwapa vijana hao wa Stephen Keshi nguvu za kuruka mbele huku wakisubiri kivumbi muhimu cha Alhamisi dhidi ya Uruguay.
Mashabiki 20 187 pekee ndio waliofika uwanja uliokarabatiwa wa Estadio Mineirao lakini walisikika sana wakiunga mkono Tahiti, ambao walipata jaribio la kwanza la kulenga goli kwenye mechi kupitia Vincent Simon.
Bahati iliwaponyoka wanyonge hao muda mfupi tu baadaye, hata hivyo.
Baada ya mpira kumgonga refa Joel Aguilar, Echiejile alitoa kombora la kujaribu bahati ambalo liligonga Tehau na nahodha Nicolas Vallar na kumpiga chenga golikipa wa Tahiti Xavier Samin.
Oduamadi aliongeza mawili zaidi, baada ya kuchenga kwa ustadi na kufunga dakika ya 10, kabla ya kufunga la pili baada ya Samin kutema mpira wa chini ulioandaliwa na Ahmed Musa.
Nigeria walifanya kazi ya ziada hata hivyo kudhibiti mechi, huku Musa akikosa wavu mbele ya goli tupu kabla ya Anthony Ujah na Sunday Mba wote wawili kumwezesha Samin kuokoa mipira yao wakiwa na nafasi wazi za kufunga.
Tahiti walikuwa tayari wameshuhudia mmoja wa wachezaji wao wa soka ya kulipwa, Marama Vahirua, akitoa kombora ambalo nusura liende ndani lakini likatoka nje kupitia juu ya goli, na walitishia kubadilisha mambo huku Steevy Chong Hue akigonga mpira nje kwa kichwa kutoka kwa mpira alioandaliwa na Ricky Aitamai.
Musa alikosa nafasi tena hatua 12 mapema kipindi cha pili, kabla ya goli ambalo Tahiti walikuwa wakisaka kwa udi na uvumba kuwasili dakika ya 54.
Bahati ilimwangukia Tehau, ambaye alitumbukiza mpira uliotoka kwa kona iliyopigwa na Vahirua hadi karibu na mlingoti na kupelekea wachezaji wenzake kushangilia sana.
Bao hilo pia liliibua shangwe kutoka kwenye benchi, huku kocha Eddy Etatea akiruka na mikono yote juu hewani, lakini siku ya Tehau iligeuka na kuwa mbaya pale dakika ya 68 alipojifunga na kurejesha uongozi wa Nigeria wa mabao matatu.
Oduamadi alifunga bao kutoka mpira alioandaliwa na Brown Ideye aliyetoka benchi na kukamilisha mabao yake matatu dakika ya 76, huku Echiejile akiongeza la sita muda mfupi baada ya Tahiti hatimaye kukoza nguvu za kujilinda.