come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

#WATUMISHI HEWA: RAIS MAGUFULI ATENGUA UTEUZI WA MKUU WA MKOA WA SHINYANGA

Na Elias John.

RAIS wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dk.  John Pombe Joseph Magufuli, ametengua uteuzi wa aliyekuwa mkuu wa Mkoa wa Shinyanga mama Anne Kilango Malecela.

Rais Magufuli amefikia uamuzi huo baada ya mkuu huyo wa Mkoa kutangaza kwenye vyombo vya habari kwamba Mkoa wake hauna wafanyakazi hewa jambo halikuwa na ukweli wowote.

Magufuli amesema baada ya kupata habari kwamba Mkoa wa Shinyanga hauna wafanyakazi hewa amejiuliza sana ijayo kama habari ni za kweli au la,  ndipo alipopata safari kutembelea mikoa ya huko akatatuma vijana wake kufuatilia jambo hilo.

Katika ripoti ya vijana wake Rais Magufuli     ameambiwa kwamba katika Mkoa wa Shinyanga Kuna wafanyakazi hewa 45 na katika Idadi hiyo bado kuna wilaya kama mbili za Mkoa huo bado zinaendelea kufanyiwa uchunguzi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotua mezani kwa Rais imesema kwamba katika Mkoa huo wilaya ambazo uchunguzi bado unaendelea ni pamoja na wilaya ya Ushetu na Shinyanga vijijini ambapo uchunguzi ukikamilika Idadi hiyo ya wafanyakazi hewa inaweza ikaongezeka.

Rais Magufuli ameongeza kwa kusema kuwa ameshangazwa na mkuu huyo wa Mkoa kwa kusema uongp wakati hakuna adhabu yoyote itakayotolewa iwapo itagundulika Mkoa una wafanyakazi hewa.

Aidha Rais Magufuli amesikitishwa na kitendo cha wafanyakazi hao hewa kulipwa zaidi ya Tsh. Milioni 336 pesa ambazo zingesaidia kutatua kero mbalimbali za wananchi.