Wapo pia baadhi ya waandishi wa habari za michezo ambao hutumia vibaya kalamu zao na kushindwa kuwapasha vizuri habari mashabiki wa vilabu hivyo.
Wanagombanisha kwa kuandika uongo ama kutotathimini vema vyanzo vya habari, takribani miaka 10 sasa sijasikia au kuona usajili ukihusisha kuchukuliana wachezaji kutoka Yanga kwenda Simba au kutoka Simba kwenda Yanga.
Ninavyoona sasa ni janja tu ya michezo, ukweli halisi Simba au Yanga hakuna timu iliyochukua mchezaji wa mwenzie, hizi timu nazifahamu vizuri hasa kwa fitina zao katika mchezo wa soka.
Simba na Yanga nazifananisha na klabu za Manchester United na Liverpool za England ambazo zimewekeana mkataba wa kutochukuliana wachezaji wao.
Siku zote timu hasimu hupenda kuhujumiana ndani na nje ya uwanja, Ujerumani kuna vilabu hasimu Bayern Munich na Borrusia Dortmund, timu hizo hazichukuliani ovyo wachezaji.
Michael Owen mchezaji kipenzi aliyepata kutamba Liverpool na kuitetemesha dunia alilazimika kuihama klabu yake hiyo na kutua Real Madrid ya Hispania ambapo baadae akajiunga kiurahisi Man United.
Isingewezekana Man United kumpata Owen akitokea Liverpool, Hata usajiri wa Robert Lewandowski una mizengwe ndani yake, Nyota huyo anayetamba na Dortmund anajiunga na Bayern baada ya kumalizika mkataba wake.
Mwaka jana klabu ya Yanga iliandamwa na mahasimu wao hasa baada ya kufanya usajiri ulioelekea kuiliza Simba, Yanga ilisajili Nyota watatu Juma Kaseja, Emmanuel Okwi, na Kiungo chipukizi wa Ruvu Shooting Hassani Dilunga, Usajili wa Okwi na Kaseja ndio uliowaumiza sana Simba Ikizingatia Nyota wao ni vipenzi ndani ya klabu hiyo Yenye Makazi yake mtaa wa Msimbazi.
Kufanya vibaya kwa kipa Abel Dhaira katika mzunguko wa Kwanza wa ligi kuu uliopelekea Simba kuishia Nafasi ya nne na kusababisha kutimua benchi lake la ufundi lililokuwa chini ya Abdallah `King` Kibadeni na Msaidizi wake Jamhuri Kihwelo Julio`.
Wakati Dhaira akishindwa kuibeba Simba macho ya wanasimba yalielekezwa kwa kipa wao wa zamani Juma Kaseja, Kaseja anakumbukwa na Simba kutokana na mchango wake muhimu alioutoa kwa muda usiopungua miaka 9.
Simba ilisubiri dirisha dogo lifunguliwe ili iweze kumrejesha,Tayari kipa huyo alianza kujifua katika mazoezi ya Simba B yakisimamiwa na Seleman Matola.
Yanga ikafanya umafia baada ya kumpa mkataba wa miaka miwili, Usajili huo uliwaacha Simba Vinywa wazi, ikafunga hesabu zake kwa kumchukua mshambuliaji anayehusudiwa zaidi Msimbazi Emmanuel Okwi.
Okwi alishauzwa na klabu yake ya Simba hivyo hakuwa mchezaji wa Simba, Klabu ya Etoile Du Sahel ya Tunisia ndiyo iliyomnunua Hata hivyo klabu hiyo ilishindwa kummiliki Okwi ambapo walishindwa kumlipa mshahara wake wa Miezi mitatu na mchezaji huyo kuishitaki timu FIFA.
Mbali na kupeleka malalamiko yake FIFA, Klabu yake ya zamani Simba ilikuwa haijalipwa fedha za mauzo ya Okwi ambapo nayo ilifungua Kesi FIFA Kutaka ilipwe fedha zake.
Sc Villa ya Uganda ilipewa haki ya kumtumia Okwi na ilipewa hati maalum ya kuwa naye miezi sita baada ya hapo Okwi atakuwa huru kuichezea timu yeyote aitakayo.
Ndipo Yanga ilipofanikiwa kumnunua Okwi kwa Sc villa, Yanga ilivunja mkataba wa miezi sita na kuongeza Miwili hivyo imemnunua kwa miaka miwili na nusu sasa Okwi ni mali ya Yanga.
Kabla ya hapo klabu ya Yanga ilipata kuchukua wachezaji wengine waliopata kuichezea Simba nyota hao ni Athumani Idd `Chuji` Kelvin Yondani, Ally Mustapha 'Barthez' Deogratus Munishi 'Dida' na Mrisho Ngassa.
Tuanze na Chuji, Yanga ilimsajili Chuji baada ya kumalizika kwa mkataba wake Simba, hivyo alikuwa huru sawa na Ally Mustapha `Barthez` ambaye hakuwa tayari kuendelea kusugua benchi Simba. Barthez alilazimika kuhamia Yanga baada ya kumalizika kwa mkataba wake.
Mrisho Khalfan Ngassa:
Usajili wa Ngassa unafanana na hao wengine , Ngassa alikuwa na mkataba na klabu ya Azam ambayo nayo ilimnunua kutoka Yanga.
Simba ilipewa kwa mkopo ili kunusuru kiwango chake, Azam isingeweza kumtumia nyota Huyo kufuatia kitendo chake alichokifanya cha kuibusu jezi ya Yanga wakati wa michuano ya klabu bingwa Afrika mashariki na kati mwaka Juzi.
Kelvin Yondani:
Yanga ilifanikiwa tena kumnasa beki kisiki tegemeo la Simba, Usajili wa Yondani ulizua utata mkubwa, lakini mkataba wa beki huyo na Simba ulimaliziaka.
Hapo utagundua kuwa Yanga haikuchukua mchezaji yeyote kutoka Simba, Deo Munishi naye alitua Yanga akisajiliwa huru, Munishi alitokea Azam Fc ambayo nao ilimchukua toka Mtibwa Sugar.
Hata Simba nao wamefanya usajili wa kuwaduwaza Yanga, mwishoni mwa mwaka jana Simba ilimchukua Ivo Mapunda ambaye aliwahi kuichezea Yanga.
Lakini Simba ilimchukua mchezaji huyo akiwa huru, Mapunda alimaliza mkataba wake Gor Mahia ya Kenya ambayo nayo ilimchukua kutoka Bandari ya Mombasa.
Ivo aliwahi kuichezea Prisons ya Mbeya na kutua Moro United ambapo Yanga ilimuona, Mapunda ilienda St George ya Ethiopia Klabu hajarejea nchin ambapo alitua African Lyon.
Usajiri wa Mapunda unaonyesha kuwa ni mchezaji huru na sio wa Yanga, sawa sawa na Yaw Berko, Berko aliichezea Yanga kwa misimu mitatu na mkataba wake ulipomalizika tu aliondoka kwenda kwao Ghana.
Simba ilifanikiwa kumsainisha kwa miezi sita, Hivyo usajili wake unakuwa huru.
Mbali na usajili huo wa Ivo Mapunda na Yaw Berko, Simba iliwahi kumchukua Kiggi Makassi ambaye ni majeruhi kwa sasa, mkataba wa Kiggi Makassi na Yanga ilipomalizika akajiunga na Simba.
Ili ujue vilabu hivyo mwiko kuchukuliana wachezaji Yanga ilijalibu kumsajili beki kisiki wa Simba katika miaka ya tisini Deo Njohole 'OCD'.
Simba walichukia na kuamua kumfungia miaka mitata asicheze soka ukawa mwisho wake, ni haramu mchezaji kutoka Simba kwenda Yanga.
Iliwahi kutokea miaka ya tisini na madhara yake yakaonekana, inakumbukwa kuwa Ezekiel Greyson 'Jujuman' alijaribu kuihama Simba na kutua Yanga lakini msimu uliofuata alirejea Simba.
Likumbukwe sekeseke la Victor Costa 'Nyumba' ambaye alichezea kwa mafanikio makubwa Simba, Yanga wakamsajili lakini kilichowakuta!