BAADA ya kumsajili Juan Mata, kocha wa Manchester United, David Moyes amesema kwamba huo ni mwanzo, mengi mazuri yanakuja na ameweka bayana mpango wa kusajili nyota wengine wawili.
"Huu ni mwanzo wa mengi yanayokuja. Nasonga mbele, Juan akiwa mwanzo wa harakati zangu,"alisema.
Wasaka vipaji wa United waliwaangalia wachezaji Filipe Luis na Diego Costa wakiisaidia Atletico Madrid kushinda 4-2 dhidi ya Rayo Vallecano jana.
Juan Mata anatarajiwa kuanza kuichezea United katika mechi dhidi ya Cardiff City kesho baada ya kusajiliwa kwa dau la Pauni Milioni 37.1 kutoka Chelsea.