Umoja wa wanasalamu Dar es Salaam na Pwani wameazimia kufanya uchaguzi wao hivi karibuni ambapo wametangaza fomu za kugombea uongozi kuwa ziko tayari kuanzia sasa, Pia wameweza wazi masharti ya kugombea uongozi ni lazima uwe mwanachama.Akizungumza na mwandishi wa habari hizi juzi, Afisa habari wa umoja huo Salum Mfunga (Pichani kushoto
'Fomu za kugombea uongozi zinapatikana kwa mweka hazina wetu Mama Double S Vingunguti jijini, Pia wale ambao wanataka uanachama wanaweza kumuona huyo huyo mweka hazina ili aweze kuwapatia kadi haraka', alisema Mfunga.
Aidha Mfunga amedai kuwa ni nafasi kwa watu wengine kuchukua fomu za uongozi ili kuondoa malalamiko kuwa umoja huo unaongozwa na watu wachache, 'Nafasi zipo nyingi na mtu anayetaka uongozi anaweza kuja kuchukua fomu' alisistiza.
Watu kadhaa wamethibitisha kuchukua fomu akiwemo aliyekuwa mwenyekiti wa zamani wa umoja huo Said Kikoti na Peter Tosh Boy ambaye anawania nafasi ya uenyekiti kuchuana na Kikoti