![]() |
|
|
|
Gor Mahia walizidi kutamba katika kilele cha jadwali ya
Ligi Kuu Kenya baada ya kuzima mwangaza wa Western Stima 2-0 katika uga
wa City Stadium, Jumapili.
Nyota aliyebobea, Rama Salim, aliwapa wana K’Ogalo uongozi dakika tano tu baada ya mechi hiyo kuanza baada ya kulemea kipa wa Stima, Benroberts Mandela na mkwaju safi wa adhabu.
Ilipotimia dakika 33, kiungo staa wa Gor, Paul Mungai Kiongera, aliwasisimua mashabiki baada ya kufunga goli la hali ya juu kutokana na makosa katika ngome ya Stima huku akinufaika kutoka usaidizi wa Salim.
Lakini sherehe za kiungo huyo zilizojaa madaha zilikashifiwa vikali na kocha Bob Williamson baada ya Kiongera kuvua jezi lake na kupata kadi ya njano.
Golikipa wa K’Ogalo, Jerim Onyango, alidhihirisha umahiri wake pale alipokoa mkwaju mkali kutoka kiatu cha Mike Simiyu.
Huu ulikuwa ushindi wa pili mtawalia katika ligi wa mkufunzi Williamson na ulishuhudia vijana wake wakifungua mwanya wa alama tano katika kilele cha ligi.