come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

MAWAKALA WA WACHEZAJI NAO KUFANYA MTIHANI WAO SEPT 26

Mtihani wa uwakala wa wachezaji na uwakala wa mechi wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) utafanyika Alhamisi ya Septemba 26 mwaka huu saa 4 kamili asubuhi kwenye ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).


Kutakuwa na jumla ya maswali 20 kwenye mtihani huo, 15 yanatoka FIFA kuhusiana na kanuni za kimataifa za mpira wa miguu na matano yatatoka TFF kuhusiana na kanuni mbalimbali zinazotawala mchezo huo nchini.

Kwa ambao wangependa kufanya mtihani huo utakaokuwa katika lugha ya Kiingereza ambayo ni moja kati ya lugha nne rasmi za FIFA wanatakiwa kujisajili TFF kwa ada ya dola 50 za Marekani ambapo watapewa utaratibu na maeneo ambapo mtihani huo unalenga.

Mtihani huo utafanyika saa 4 kamili asubuhi, na muda wa kufanya mtihani hautazidi dakika 90.

Mpaka sasa Tanzania ina mawakala watano wa wachezaji wanaotambuliwa na FIFA. Mawakala hao ni John Ndumbaro, Mehdi Remtulla, Ally Saleh, Yusuf Bakhresa na Said Tully.