come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

MBUYU TWITE KUREJEA UWANJANI AGOSTI

Mbuyi Twite
Klabu ya Yanga imesema kuwa mchezaji wake wa kimataifa wa Rwanda, Mbuyi Twite ambaye amepata jeraha la goti wakati timu hiyo ikiwa kwenye ziara kanda ya ziwa, atakuwa tayari kuichezea timu hiyo ndai ya siku 28.


Twite aliumia goti katika ziara hiyo na kutokana na kushindwa kufanya mazoezi na wachezaji wenzake mpaka sasa akiwa kwenye uangalizi wa daktari wa timu, Nassoro Mutuzya, palikuwa na wasiwasi kuwa kuwa asingeweza kuwahi ufunguzi wa msimu Agosti 24.

Lakini akizungumza jana, Afisa Habari wa Yanga Baraka Kuzuguto, alisema Twite anaendelea vizuri na matibabu na Mutuzya amethibitishiwa kuwa atakuwa fiti kabla ya tarehe hiyo ya kuanza kwa msimu mpya wa ligi kuu ya Bara.

Alisema awali walidhani majeraha aliyoyapata mchezaji huyo ni makubwa lakini baada ya uchunguzi wa kina imeonekana atawahi kupona kabla ya mechi ya kwanza ya ligi kuu.
"Kweli awali tulijua ameumia sana na tukawa na hofu pengine hatakuwa tayari kwa michezo ya mwanzoni ya ligi," alisema Kizuguto.

"Lakini daktari ametuhakikishia anaendelea vizuri na pengine wiki moja au mbili zijazo akaanza mazoezi mepesi na mpaka kufikia ligi kuanza atakuwa yupo fiti."

Yanga itaanza kutetea uibngwa wake wa 23 wa Bara Agosti 24 kwa kupambana na timu iliyopanda daraja ya Ashanti United.

Aliwataka mashabiki wa klabu hiyo kutoa hofu kwa sababu kama "mambo yatakwenda vizuri zaidi", Yanga inataraji mchezaji huyo atakuwemo uwanjani siku ya mchezo wa Ngao ya Hisani dhidi ya Azam, Agosti 17.
Mchezo huo ni ishara ya ufunguzi wa pazia jipya la ligi kuu ya Bara.

Katika hatua nyingine, Afisa Habari wa Yanga Baraka Kuzuguto, alisema uongozi wa klabu hiyo unajiandaa kuitoa timu hiyo nje ya mkoa wa Dar es Salaam kwa ajili ya kuweka kambi ya kujiandaa na mchezo dhidi ya Azam na maandalizi ya ligi kuu kwa ujumla.

Wakati Simba ikiwa tayari imepiga kambi Bamba Beach Dar es Salaam, kikosi cha Yanga huenda kikaenda mjini Zanzibar au Bagamoyo kwa ajili ya maandalizi hayo.