Siku za hivi karibuni mimchezo ilionekana kupoteza mwelekeo hasa baada ya kutokuwepo kwa wanamichezo wenye nia ya kuendeleza, Vijana walianza kujiingiza kwenye matumizi mabaya ya dawa za kulevya na kupelekea mkoa huo kupata sifa mbaya.
Historia ya Tanga inaonyesha kuwa mji huo umetawaliwa na ustaarabu wa kipekee lakini sasa ulianza kutoweka, Carlos Hiza kijana aliyejitosa kwenye masuala ya siasa na kupata udiwani katika kata ya usagara jijini Tanga ameamua kuwa mwanamichezo wa kweli ili kufufa na kuendeleza michezo mkoani hapo.
Akizungumza na mwandishi wa makala hii hivi karibuni, Carlos Hiza (Pichani), amesema kuwa ameamua kuanzisha mashindano ya soka ya Carlos Power Cup kwa lengo la kuleta msukumo wa kuendeleza soka mkoani hapo.
Aanadai michuano yake aliyoianzisha ambapo sasa imefikia hatua ya fainali itakayochezwa siku ya jumapili imeleta hamasa kubwa kwa wakazi wa Usagara na maeneo jirani, Pia amepanga kuanzisha mashindano mengine ya basketiboli kwa wanawake na wanaume.
HIZA AIELEZEA LIGI YAKE
Ligi yangu inaitwa Carlos Power Cup ni ligi ya kata ya Usagara jiji la Tanga imeanza tarehe 19/5/2013 ikishirikisha timu 18 ambazo ni Pentgon, Mtotesho, Veteran FC, Kingstone FC, Kausha FC, Al Shaabab SC, Mong'oo, Umoja ni nguvu FC Blant, Flant Corner, Mitundani FC, NdUlichwaka, Moro FC, Bafana Bafana, Manyigu na Lugongo FC.
Timu zilizoingia robo fainali ni pamoja na Mtotesho FC, Umoja ni nguvu, Pentagon, Bafanabafana, Mong'oo na Blant. Zilizoingia nusu fainali ni Pentagon, Mtotesho, Umoja ni nguvu na FC Mong'oo.
Na timu zilizoingia fainali ni pamoja na Pentagon FC na Umoja ni nguv ambazo zitakutana siku ya jumapili kwenye uwanja wa Bandari jijini Tanga,
Nikiwa kama diwani wa Usagara jijini Tanga nimeanzisha ligi hii kwa lengo la kukuza vipaji vya mpira wa miguu kwa vijana wetu na kuwaunganisha pamoja, aidha kuwajenga kiafya kwa kushiriki michezo na kuleta mahusiano mema na upendo.
Matarajio yangu ya baadaye ni kuanzisha michuano ya mpira wa kikapu kwa vijana wa kike na kiume, mashindano ya riadha nk, alisema Hiza ambaye ni diwani mwenye ndoto za kweli kuendeleza michezo jijini Tanga.
Baadhi ya wakazi wa Tanga wamemsifu diwani huyo kwa mikakati yake ya kukuza soka Tanga, Wakizungumza kwa nyakati tofauti Hashim Fimbo amedai kuwa Usagara ilisahaulika kisoka kwa muda mrefu lakini Hiza amekuwa mkombozi.
Amedai kuwa vijana sasa watapata fulsa ya kuonyesha vipaji vyao kutokana na michezo mbalimbali itakayoanzishwa na diwani huyo, Naye Fai Muya ambaye ni mkazi wa Tanga amemsifu diwani huyo wa CCM kwa moyo wake wa kuinua michezo Tanga.
Huyo ndiyo Carlos Hiza ambaye ni mwanamichezo jijini Tanga je ataweza kuendeleza michezo au nguvu za soda, Basi tusubiri kisha tuone, Tuonane wiki ijayo
Makala hii kwa mujibu wa gazeti la Kabumbu