
Rais mteule wa Iran Hassan
Rouhani anaapishwa katika sherehe mjini Tehran ambapo atapewa idhini ya
kiongozi wa kidini nchini humo, Ayatollah Ali Khamenei.
Rouhani ambaye alikuwa mpatanishi kwenye
mazungumzo ya mradi wa nuklia wa Iran, alishinda uchaguzi wa urais
nchini Iran katika duru ya kwanza.
Wakati wa kampeni zake rais huyo mteule aliahidi
kuleta mabadiliko ya kijamii na kiuchumi, na alisema ataimarisha
uhusiano kati ya taifa hilo na jamii ya kimataifa ambao uliharibika
zaidi wakati wa utawala wa Rais Mahmoud Ahmedinejad.