MAISHA ya beki wa zamani aliyepata kuzichezea Yanga, Simba na Taifa Stars Amir Mafthan kwa sasa yapo shakani hasa baada ya klabu ya Simba kumtosa jumla na kushindwa kumlipa fedha zake alizokuwa akiidai mwaka jana kabla hajatimuliwa.
(Pichani, Amiri Maftaha kushoto akiwa na rafiki take baada ya kuachana na soka)
Mwandishi wetu alizungumza na nyota huyo kupitia mitandao ya kijamii hivi karibuni ambapo Maftah alijutia uamuzi wake wa kucheza soka licha ya kujifariji kuwa amenufaika na mambo machache kupitia mchezo huo, hata hivyo kwa uchunguzi uliofanywa na mtandao huu umegundua kuwa Maftah anajuta kucheza soka.
Umri wake bado mdogo na alihitaji kuendelea na soka lakini majuto yaliyomkuta imembidi ajitumbukize kwenye shughuri nyungine ili mradi aweze kuendesha maisha yake ya kila siku, nyota huyo alipata kutamba katika klabu ya Yanga kabla ya kutemwa kwa madai kuihujumu Yanga kilainapocheza na Simba.
Lakini alipokuwa Simba alitamba kwa kipindi kifupi kabla hajatimuliwa kwa madai ya utovu wa nidhamu, lakini ikagundulika kuwa Simba ilimdhulumu fedha zake na kumfanya ashindwe kusajiliwa tena na klabu hiyo sambamba na nyota wengine watano, Maftah alimwambia mwandishi wetu kuwa ameamua kukaa chonjo na kufanya kazinyingine ingawa hakuweka wazi.